Thursday, 31 January 2013

PRISCA KALORY A.K.A MAMA KIJACHO

MSINULIZE KWA NINI ILA NIMEJISIKIA KUTUNDIKA PICHA ZAKE HAPA JAMANI

SMILE HILO MAMA KIJACHOOOO

TUMBO SASA KUBWAAAAAA MPAKA KAWA MFUPI ZAIDI

AMEJICHOKEAJEEEEEEEE


WACHA WEEEE, ANDEZHA WEWEEEEEE!!!

MY SUPER WOMAN, MY HERO, MY MUM

I MISS HER JAMANI, IT'S LIKE AGES TO ME MUM. MISS YOU MUCH MUM

Tuesday, 29 January 2013

NAMSHUKURU MOLA MWINGI WA REHEMA NA MWENYE KUREHEMU

NINA KILA SABABU YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA LILILOTOKEA KWENYE MAISHA YANGU. LOLOTE LILILONIFIKA NI KWA MAPENZI YAKE. NAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA AMEENDELEA KUNITIA NGUVU NA KUNILETEA MARAFIKI NA NDUGU WANAONIFARIJI KILA KUKICHA. NAWAPENDA NDUGU ZANGU, FAMILIA YANGU NA MARAFIKI ZANGU. NIMEPEWA AU TUMEPEWA ZAWADI KUBWA YA KUWA NA NDUGU NA MARAFIKI WANAOTUPENDA KWA DHATI. ASANTE MUNGU KWA ZAWADI HII KUU NITAENDELEA KUIENZI KWA MOYO NA AKILI ZANGU ZOTE ULIZONIJAALIA. REST IN PEACE MAMITO.






Monday, 28 January 2013

HII NI KWA AJILI YA MARAFIKI ZANGU WAPENZI

MY DEAR FRIENDS, SIJUI NIZUNGUMZE AU NIANDIKE VIPI ILI MPATE MAANA HALISI YA KILE NINACHOTAKA KUZUNGUMZIA. KIKUBWA NINACHOWEZA KUSEMA NI ASANTENI SANA KWA UPENDO MLIOUONYESHA KWANGU, MLINIKIMBILIA PALE NILIPOKUWA NAWAHITAJI KULIKO KITU KINGINE, MLINIFARIJI KUPITA HATA NILIVYOWAHI KUFARIJIWA NA MLIKUWA KARIBU YANGU KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE. SISEMI KWA WALE WALIOWEZA KUJA TU ILA HATA WALE AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WALIKUWA KARIBU NA MIMI INGAWA HAWAKUAAJILIWA KUFIKA KWENYE MAZISHI. MIMI SIWEZI KUFANYA AU KUONGEA CHOCHOTE KWENYE HILI MLILOLIFANYA ILA NAMUOMBA MUNGU AWAAJALIE KILA LILILO LA KHERI NA KUWEKA WEPESI KWENYE KILA LILILO GUMU. KWANGU MMEKUWA KAMA NYOTA INAYOAMBATANA NA MBALAMWEZI KILA SIKU. MMENISIMAMIA NA BADO NAAMINI MNAENDELEA KUNISIMAMIA, ASANTENI SANA KWANI MMEKUWA ZAIDI YA NDUGU KWANGU. MUNGU ATUSIMAMIE WOTE ILI UPENDO HUU USIJE VUNJIKA KAMWE INGAWA KUNA VITU VINAVYOSUKUMA HILO LITOKEE. NAWAPENDA SANA NA NAMUOMBA MUNGU ANIJALIE MOYO SAFI WA KUTUNZA UPENDO HUU NDANI YANGU.

Wednesday, 23 January 2013

REST IN PEACE MAMA




Sijui nianzie wapi, Kwangu mimi ni mpiganaji wa hali ya juu, alikuwa zaidi ya mama, rafiki yangu, shoga yangu, msiri wangu, mshauri wangu na mpiganaji wangu (greatest mother in the world). Mama yangu ndio alikuwa kila kitu kwangu. Hakuna nililokuwa naweza kufanya bila yeye, hapa nilipo nisingefika bila yeye. nashindwa kupata neno sahihi la kuandika au kuelezea wasifu wa mwanamke huyu. Nimepoteza lulu katika maisha yangu, nimepoteza ngao muhimu na mhimili mkuu katika maisha yangu. Natamani japo angerudi au nimuone tena ili tuweze kufanya yale tuliyozoea kufanya. Tucheke pamoja, tupike pamoja au tulie pamoja wakati mwingine. Mama, nitawezaje bila wewe? Nitafanye bila wewe? Nianzie wapi mama? nifanye nini mimi mama? ulikuwa unajibu maswali yote haya ila sasa sina wa kunijibu maswali yangu, sina wa kufanya ya kwangu maana ulikuwa unafanya kila kitu. Tarehe 12/01/2013 ilikuwa siku ngumu sana kwangu, sikuamini kilichotokea na bado siamini. Wakati mwingine huwa nahisi nipo kwenye ndoto ndefu na ya kutisha ambapo itaisha nitaamka na kukupigia simu mama yangu na uanze kuleta utani wako wa kila siku ambao unanifanya nicheke mpaka walio karibu wanione labda nachanganyikiwa. Eeeeh Mungu nitie nguvu mimi na familia yangu hasa mdogo wangu mpenzi Anna ambaye mama alikuwa kama roho yake, nitafanya nini na Anna mimi, nitaanzia wapi na Anna mimi? Mama huu ni mtihani mwingine ulioutupa kwenye mikono yangu. Umeniachia ya kwangu lakini bado umeniachia ya Anna pia. Bado nahitaji msaada wako mama peke yangu siwezi. Namuomba Mungu anijaalie subra na anipe wepesi kwa kila jambo. Najua bado upo pamoja nasi kama ulivyokuwa ingawa kwa sasa itakuwa tofauti. Mama yangu, nyota yangu, nguzo yangu, kipenzi cha roho yangu, kama nilivyokuheshimu wakati wa uhai wako sitaacha kufanya hivyo milele. Kama nilivyokupenda kipindi cha uhai wako sitaacha kufanya hivyo daima. Nilikupenda, nakupenda na nitakupenda milele mpaka mwisho wa maisha yangu tutakapokutana tena. Naomba Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi na akulaze mahali pema peponi kipenzi changu, aaamen.


 

My super woman and Anna

Mum, Anna & Dad hii ilikuwa November 2012