Sunday, 12 January 2014
IN LOVING MEMORY OF MY SUPER WOMAN, HERO, SHOGA AND ADORABLE MOTHER. IT'S ONE YEAR MAMA
IMETIMIA MWAKA MMOJA LEO MAMA TOKA ULIPOLALA USINGIZI WAKO WA MILELE. NI MWAKA MMOJA MGUMU SANA KATIKA MAISHA YETU MAMA, NI MWAKA ULIOKOSA MWELEKEO TOKA TULIPOKUKOSA MAMA MPENZI. KUNA WAKATI HUWA NAITA KWA SAUTI BILA MAFANIKIO WALA DALILI YA KUITKIWA NAWE. UKO WAPI MAMA YANGU JAPO UNIITIKIE KWA MARA MOJA YA MWISHO ILI NIWEZE KUSEMA LILE NILILOSAHAU KUSEMA SIKU ZOTE MAMA ETI KWA KISINGIZIO NASUBIRI SIKU MAALUM ILI NISEME?? WAPENDWA KAMA BADO MAMA YAKO YUPO HAI HEBU MWAMBIE KILA KITU UNACHOHISI UNATAKA AJUE KUTOKA KWAKO ILI YASIJE YAKAKUKUTA KAMA YANAYONIKUTA MIMI SASA, NATAMANI SANA KUSEMA ILA SINA PA KUSEMEA, NTAMWAMBIA NANI?? HIVI MAMA UNAKUMBUKA KUWA ILIKUWA LAZIMA TUONGEE KILA BAADA YA SIKU MOJA?? NA IKITOKEA NIKAKAA KIMYA SIKU MBILI UTANIPIGIA NA KUNILAUMU KWA NINI NIMEKAA KIMYA, NA KUSEMA KUWA MIMI MAMA MBAYA?? MAMA, IMEKUWA ZAMU YAKO KUKAA KIMYA KWA MWAKA MZIMA SASA? NATAMANI SANA KUKUPIGIA MAMA JAPO NISIKIE SAUTI YAKO. NIMEMISS KILA KITU KUTOKA KWAKO MAMA. NINA CLIP AMBAYO ILIREKODIWA SIKU NYINGI KIDOGO TOKA OLIVER AKIWA NA MIEZI MIWILI NDIO KUNA SAUTI YAKO HUKO, HUWA NAIRUDIA KILA NINAPOPATA NAFASI ILI TU NIISIKIE SAUTI YAKO. EEEEH MUNGU HAYA MAWAZO YA KUTAKA KUMPIGIA MAMA YANGU LINI YATATOKA KICHWANI MWANGU??? SIO KWAMBA NAJILAUMU ILA IMEKUWA NGUMU SANA KWANGU MUNGU. NISAIDIE BABA. MAMA NILIWAHI KUAMBIWA KUWA MAREHEMU WETU WANAJUA KILA TUNACHOFANYA, KWA MAANA HIYO UNAONA KILA KITU TUNACHOFANYA NA KUPITIA NA BADO UMEKAA KIMYA MAMA?? NINA HAKIKA UNGEKUWEPO LABDA TUSINGEPITA HUKU, SIO KWAMBA NAKUFURU ILA ULIKUWA ZAIDI YA MAMA KWETU SOTE. SIJUI NIITEJE ILI UWEZE KUSIKIA SAUTI YANGU TENA MAMA YANGU, NAHISI IMESHAANZA KUFUTIKA KICHWANI MWAKO NA KUNA WAKATI HUWA NAHISI LABDA IMEANZA KUPOTEZA THAMANI HIVII. NIITIKIE BASI MAMA YANGU MPENZI ILI UNITOE KWENYE ILI JAKAMOYO MAMA. NAHISI KUSHINDWA KUENDELEA MAANA MACHO YANGU YAMEJAA MACHOZI KWA KUONA KAMA NAONEWA VILE. SIO KWAMBA NAKUFURU ILA MAMA MCHUNGU JAMANI NA HASA AKIONDOKA UKIWA MKUBWA NA ULIYEJUA NINI MAANA YA PENZI LA MAMA. NARUDIA TENA KAMA MAMA YAKO YUPO HAI LEO HII UNAPOSOMA HILI PLEASE MPE KILA LINALOSTAHILI KUPEWA MAANA KUNA SIKU UTAHITAJI NAFASI HIYO NA HUTAIPATA. NA KWALE WALIOPOTEZA MAMA ZAO NAWASIHI SANA MSIACHE KUWAOMBEA MAANA ROHO YA MAMA NI KAMA DHAHABU NA UKUSIKIA POPOTE ALIPO. MUNGU NAOMBA ILAZE ROHO YA MAMA YANGU KIPENZI MAHALA PEMA PEPONI, MPE NGUVU BABA YANGU MPENZI MAANA KUNA WAKATI HUWA NAHISI KUWA BADO HAJAKAA SAWA MPAKA LEO. ISIMAMIE FAMILIA YANGU, PLEASE NDUGU ZANGU WE HAVE TO STAY STRONG. NAKUPENDA SAN MAMA YANGU, NAKUHESHIMU SANA MAMA YANGU NA NAKUTHAMINI SANA MAMA. TULIKUWA NA BAHATI SANA KUKUPATA WEWE KAMA MAMA YETU.
REST IN PEACE MAMA KATIBU
31-08-1950 --- 12/01/2013
Wednesday, 1 January 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)