NINA KILA SABABU YA KUMSHUKURU MUNGU KWA HATUA HII KUBWA ALIYONIWEZESHA KUIFIKIA, HAPA NILIPO MIMI NI NEEMA YAKE TU. PAMOJA NA MAGUMU YOTE NILIYOPITIA KATIKA KUUENDEA MWAKA WANGU HUU IKIWEMO NA MARADHI, NASHUKURU KWAMBA SASA NIKO SALAMA NA NINAENDELEA VIZURI. ASANTE MUNGU KWA KUWA UMEKUWA FIMBO YANGU YA KUINUKIA KILA NILIPOANZA KUANGUKA. PIA NTAKUWA NA TABIA MBAYA KAMA SITAISHUKURU FAMILIA YANGU, BABA YANGU MPENZI AMBAYE AMEKUWA EGEMEO LANGU, KAKA ZANGU AMBAO HAWAKUCHOKA KUNIJULIA HALI KILA SIKU NA KUJUA MAENDELEO YANGU. ANDREW NA JACOB, NAWAPENDA SANA NA MUNGU AWATUNZE BABA ZANGU. MZEE MALUGU NA FAMILIA YAKE, SIJUI NIWALIPE NINI. MAMA MALUGU ULIKESHA NA MIMI USIKU KUCHA, ASANTE SANA MAMA. MUNGU AWATUNZE. DADA YANGU KIPENZI DEVOTHA, SINA LA KUSEMA ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA THAMANI ULIYONAYO MOYONI MWANGU. WEWE NI MAMA YANGU NA ITABAKI KUWA HIVYO MPAKA MUNGU ATAKAPOTUTENGANISHA. NAKUPENDA SANA MAMA YANGU. ANNA, KIBIBI, BUGUMBA, SIJUI NIKUITE JINA GANI MDOGO WANGU. ULIKUWA MKUBWA KWANGU KWENYE HIKI KIPINDI CHOTE MAMA. NAKUSHUKURU KWA KILA KITU, KWANI WEWE NDIO KILA KITU KWANGU NA NDIO MAISHA YANGU. MUNGU AWATUNZE MAANA WEWE NA DADA MLIPIGANA KIUME. KATIKA WOTE SIWEZI KUMSAHAU BEST FRIEND WANGU, RAFIKI YANGU, KIPENZI CHANGU, MUME WANGU, BEGA LANGU LA KULIA,USINGIZI WANGU, RAFIKI YANGU WA KARIBU GODFREY(STEVE). WEWE NDIYE ULIKUWA FARAJA YANGU YA KWANZA, NAHISI BILA WEWE SIJUI INGEKUWAJE BABA. ASANTE SANA KWANI ULIBEBA JUKUMU KUBWA KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE BABA KIASI AMBACHO KILA NIKIKAA HUWA NAJIULIZA NTAKULIPA VIPI. SIWEZI KUAHIDI CHOCHOTE ILA MUNGU NDIYE ATAKAYEKULIPA. ULISIMAMA NA MIMI KILA MAHALI NA KUSIMAMISHA SHUGHULI ZAKO ZOTE KWA AJILI YANGU. NILIKURUDISHA NYUMA KWENYE KAZI ZAKO ILI TU UPATE KUNIANGALIA MIMI. ASANTE SANA BABA NA MUNGU AKUBARIKI SANA. SAMAHANI KWA KUANDIKA MENGI ILA HAPA NILIPO NI KAMA MUUJIZA TU ULIOPITA KATIKA MAISHA YANGU. ASANTE SANA MUGNU.
ASANTE SANA MUNGU KWANI HII YOTE NI NEEMA TU. HAPPY BIRTHDAY TO ME
NAKUPENDA SANA MAMA MAANA BILA WEWE NISINGEKUWEPO DUNIANI NA UJUE UMENIACHA KWENYE MIKONO SALAMA. R.I.P MAMA. MISS YOU