Tuesday, 28 July 2015

MMMMMMH NO COMMENT


MMMMMMMH SISI YETU MACHO TU NA HIZI SIASA ZA BONGO.

".....CCM kuongelea ubaya wa Lowassa kwa sasa ni sawa na mtu kujichungulia nyeti zake...Chadema kuongelea uzuri wa Lowassa kwa sasa ni sawa na mtu kujitekenya na kucheka mwenyewe....Vyote vinahitaji uso usio na soni"-Edo kumwembe.

SIO KWA SABABU YA KUTETEA MASLAHI YA NCHI ILA KWA SABABU YA KUHARAKISHA KUIANGUSHA CCM?? NDIO MAANA NASEMA HAKUNA ANAYETUFAA KWA UONGOZI NCHI HII, WOTE WANAANGALIA MASLAHI YAO TU

TUNDU LISSU AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MH. LOWASSA NA KUFICHUA MENGI JUU YAKE
Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.
Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetukama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
 

Friday, 10 July 2015

IJUMAA KAREEM


 
 






HIZI PICHA NILIPIGA KIPINDI CHA RAMADHANI MWAKA JANA, NIMEZIONA TU NIKAZITAMANI.

Wednesday, 8 July 2015

HAYA MAZITO KIDOGO, KUNA UZIMA HAPA?? AU KICK.COM


Watanzania munisuport Mimi Tanzania mwenzenu...... uyo Mgandaa ni 360 watanzania wotee ni nduguu mali za watanzinia zitumiwee na wataniaa iwejee MTU from no where atuchukulie kijana wetuu mnajua Tanzania hairuhuruu urai wa nchi mbili what if diamond akiamua kufunga ndoa na zari Diamond akachukua Uraia wa South ili wamlee mtoto hamuoni atakua tumepoteza icon... muni support nimpate dai tuoanee atabakia kwetu..... nipigieni kura Mumtagg Diamond najua akiniona niko natural atanitongoza....By Baby_ake
Pia amepost picha hii na kuandika haya:Mrs and mr D..... Msinitukanee eti mnasema nimechanganyikiwa.. yes nimechanganyikiwa kimapenzi you cant tell me nothing.. yaani MTU akinivunja moyo now ntamtukama matusii yanguoni sijawahi mtukana MTU but mnanilazimisha


Basi mwenzenuu Leo nimeota niko Kitanda kimoja na Diamond ..... haha nimeonja muogo wake wa jangombe ni mtamu . .... yaani tume last 45 kiu yoote kaikata. . .. kushtuka ni ndoto but i hope. Itakua kweli. I LOVE you D
Team baby ake mpooooooooooooo?


ushahidi wa pili huu hapa 

 

Wednesday, 1 July 2015

HII NAYO KALI, DIH

RACHEL TEMU SAID!!!
 
MR-II-SUGU-NA-MTOTO-WAKE
 


Kwa kweli napenda kuwapa pongezi sana waheshimiwa Martha Mlata and Saada Mkuya kwa juhudi walizozionyesha katika kushughulikia suala la Mheshimiwa Sugu kumnyang'anya Faiza bint wao mwenye umri wa miaka miwili.
Nilikua nimenyamaza kufuatilia kwa makini hili suala lakini leo nataka niseme jambo.
Mheshimiwa Sugu wewe ni kaka yangu wa mbali kwenye familia lakini tabia zako ni ngumu kama mkaanga sumu. Na sintokutetea leo kabisaaa kwani ulilofanya sio haki. Mara ya kwanza unakutana na Faiza ulimkuta anavaa nguo anazopenda yeye, ukampa mimba ukamwambia aache kuuza duka lake utamfungulia hoteli mbeya hay yote yalikua ni changa la macho. Faiza alikua ana maisha mazuri kabla hajakutana na wewe lakini umefanfanyoko huyu dada na kustress baada ya kumjaza mimba akajifungua ukaanza tafrani bin shahidin. Ulikua hutoi hela za matumizi baada ya Faiza kujifungua kinachoniuma saana ulikua unaweza kupotea miezi mitatu hupatikani kwenye simu hujulikani ulipo na wala hujui Faiza kala nini wala Sasha kanywa nini.
Hichi ndicho chanzo cha faiza kuhama kwako na kurudi kwao kwani angekufa amesimama ndani kwako. Matuzi na fedheha ulizokua unamrushia mama Sasha zilimfika kooni ikabidi aamue kurudi kwao kwa jinsi mateso na manyanyaso aliyokua anayapata. Baada ya Faiza kurudi kwao ulikua hutoi hata ndururu kwa kumsaidia mtoto Sasha mpaka familia ilipokuweka kitimoto na kukusimanga na ndipo ulipoanza kutoa msaada kwa shingo upande. Hivi kweli na ubunge wako laki tano kwa mwezi kwenye mahitaji ya mtoto yanamsaidia nini. Kodi ya nyumba alikua anajilipia faiza mwenyewe anahangaika huku na kule aweze kumsitiri Sasha. Baada ya kuwekwa kitimoto ndio ukaona aibu ukaanza kujituntumua unatoa hela za matumizi hizo senti laki tano na hela jidogo ya ada.
Leo unakuja unampeleka Faiza mahakamani bila taarifa na kumshitaki kuwa hawezi kumlea mtoto Sasha kwa sababu ya uvaaji wake wa nguo. Hivi moja jumlisha moja uvaaji wa nguo unahusiana vipi na malezi ya Sasha basi waakina Britney Spears na akina J. Lo na akina Madonna wangenyang'anywa watoto wao. Hat siku moja Sasha hajawahi kulala njaa wala kunyanyasika matunzo aliyokua anapewa na mama yake ni ya hali ya juu ambayo hata watoto wa kawaida hawayapati. Faiza alikua analamimika asubuhi mchana unavyojigamba kwammba unamjali Sasha kwa kujiphotola mapicha na kuweka kwenye mtandao lakini ni kazi bure huna lolote Sugu zaidi ya kuleta usaga lami wako bila mafanikio.
Kinachonisikitisha huoni hata aibu leo unamchukua Sasha wakati wewe mwenyewe huwezi kumlea kwani unasafiri masaaa mia uko barabarani na kingine hujatulia hata robo wanawake kila kona ya jiji wanaomtukana Faiza kila kukicha leo ndio unataka wamleee Sasha wakati wao ni madunga yembe wanaodandia treni kwa mbele. Watamuumiza mtoto.
David Kafulila wewe nilifikiri una aakili lakini ni mburulaaaaaz.com you dont feel pity and sad jinsi Sugu anavyofanya na alivyofanya kwa wanawake wengine especially hii ya Faiza kunyang'anywa mtoto unaona haki eti mavazi anayovaa hayana maadili. Jamani jamani baasi na akina mama yeyyoo wanyang'anywe watoto kwani matiti yao yote vualaaaa nje nje mali ya serikali ya jamuhuri wa muungano. Kafulila ningekua jana bungeni ningekuchachafya kwani hujui ulisemalo na nina uhakika wewe huajlelewa na mama na ndio maana unaongea upuuzi na ushuzi ndani ya Bunge. 
CHADEMA jipangeni saaana hili suala la Sugu sio zuri na kingine mshaurini aache kuvuta msuba unamponza kwani hazimogo kaka yetu huyu na hata kwenye familia yao haieleweki so you can imagine yeye kuwa na msimamo hata wa kumlea baby Sasha.
Ukisikiliza bunge la jana nimempenda sana Mheshimiwa madame spika alivyomfunga domo kaya Kafulila kwa kuongea ujinga ndani ya bunge salute mama Makinda. Waziri Saada Mkuya naamini wazi wanawake mliopo bungeni kaeni chini mfikirie hili suala la Sugu kumnyang'anya Faiza mtoto. Sugu bila haya najua wazi umeshauriwa na ndugu yako jina na muhifadhi kwani alishaniambia wiki mbili zilizopita mkapanga jinsi ya kumchukua Sasha within a short notice. Nakwambieni sintofunga mdomo mpaka kieleweke kwani this is not acceptable na nitamtetea Faiza all the way. ARUDISHIWE SASHA WAKE. Sugu jipange jinsi ya kujenga uakaribu na mwanao kwani hajakuzoea anakuona kama uncle fulani leo unasema unamchukua. Walahi naaapa hata TAMWA tutakwenda ili mradi haki ifanyike na kuanzia leo na undugu wetu ukufe kwani huna faida kabisa zaidi ya kuleta mtafaruku kwenye familia na machungu kwenye familia ya Faiza. SHAME ON YOU SUGU. THIS IS JUST PART ONE.
TO BE CONTINUED.........

Joseph Mbilinyi leo bungeni
Kwenye kilichosikika June 25 2015 toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma ilikuwepo pia ishu ya Mbunge Martha Mlata kuanzisha mjadala kuhusu amri ya Mahakama kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi Sugu akabidhiwe mtoto wake ambae amezaa na Faiza Ally kutokana na Mbunge huyo kuonekana kutoridhwishwa na malezi ya mtoto akiwa kwenye mikono ya mama yake.
Ombi likapokelewa kwenye meza ya Naibu Spika leo June 26 2015 >>>”Nimepokea ombi maalum la kuwasilisha maombi binafsi kutoka kwa Mbunge Joseph Mbilinyi kwa hiyo namruhusu” >>> Naibu Spika Job Ndugai.
“Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo”
“Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia“
“Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika“
“Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito“
“Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge“
“Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niiwashilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
“Mashauri haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa” >>> Mbunge Joseph Mbilinyi.
 
Nimeitoa kwa Nuru The Light