Wednesday, 30 September 2015
DIH AFADHALI LABDA HESHIMA ITARUDI UWANJANI. NYOSSO AFUNGIWA KUCHEZA MPIRA KWA MIAKA MIWILI
Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya
Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Tuesday, 29 September 2015
Monday, 28 September 2015
HAKI YA MAMA NYOSO SIO MZIMA, AMDHALILISHA BOCCO MCHANA KWEUPE
Kunradhi kwa picha hii; Juma Nyosso (kushoto) akimdhalilisha mchezaji mwenzake, John Bocco mbele ya refa aliyekuwa akisuluhisha mgogoro wa wachezaji wa timu hizo
BEKI na Nahodha wa Mbeya City, Juma Said Nyosso kwa mara nyingine leo amefanya kitendo cha udhalilishaji dhidi ya wachezaji wenzake, baada ya kumtomasa makalio, Nahodha wa Azam FC, John Raphael Bocco.
Tukio hilo limetokea leo kipindi cha kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Nyosso alitumia mwanya wa refa Martin Saanya kutatua mgogoro baina ya wachezaji wa timu hizo, na kumtomasa mwenzake nyuma.
Na Bocco alionyesha utulivu na ustaarabu wa hali ya juu licha ya kuonyesha dalili zote za kukasirishwa na kitendo hicho, kwani alimfuata refa Martin Saanya kuwasilisha malalamiko yake.
Saanya hakuonekana kuyatilia mkazo malalamiko ya Bocco, ambaye alipandisha hasira na kutaka kumpiga Nyosso kama si refa huyo kuwatenganisha.
Benchi la Ufundi la Azam FC lilipeleka ushahidi wa picha kwa refa wa akiba, Soud Lila wa Dar es Salaam pia, ambaye alitoa maelekezo picha hizo zipelekwe kwa Ofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Iddi Mshangama.
Tukio hilo lilionekana kabisa kumnyima raha Bocco na kushindwa kucheza katika kiwango chake kuanzia hapo, ingawa Azam FC ilifanikiwa kushinda 2-1.
Hii inakuwa mara ya tatu kwa Nyosso kuonekana akifanya hivyo uwanjani, mara ya kwanza akiwa Ashanti United mwaka 2007 alimfanyia hivyo mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Jospeh Kaniki aliyejibu kwa kumpiga ngumi hali iliyomponza kufungiwa na TFF.
Refa Martin Saanya akiwatenganisha Bocco na Nyosso (kulia) wasipigane
Nyosso na Bocco wakirushiana maneno mbele ya refa
Mwishowe Nyosso alionekana kama kumuomba msamaha Bocco
Akarudia tena msimu uliopita akiwa Mbeya City, alipomtomasa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Elias Maguri. Kutokana na ushahidi wa picha za magazeti, Nyosso alifungiwa mechi sita na TFF.
Huku wengi wakidhani kwamba adhabu hiyo itakuwa fundisho kwake na hataweza kurudia tena, leo Nyosso ameonyesha yeye ni ‘nunda’, kwa kurudia tena baada ya kumdhalilkisha Bocco.
Wachezaji wote wa Azam FC wamekasirishwa na kitendo cha Nyosso na kiungo wa timu hiyo, Himid Mao amesema mchezaji mwenzao huyo si wa kumvumilia tena.
Azam FC leo imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 2-1 Mbeya City.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Morogoro, aliyesaidiwa na Julius Kasitu wa Shinyanga na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, mabao ya Azam FC yalifungwa na
kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 10 na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche dakika ya 52, wakati la Mbeya City lilifungwa na Raphael Alpha dakika ya 56.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 12, sawa na Mtibwa Sugar na Yanga SC, zikifuatiwa na Simba SC yenye pointi tisa.
Friday, 25 September 2015
Wednesday, 23 September 2015
IMETIMIA MWAKA MMOJA SASA MY DEAR AUNTY SANIA. R.I.P SANIA
DAH, SIKU ZINAKIMBIA SANA. SITAKI KUAMINI KAMA TAYARI UMETIMIZA MWAKA MY DEAR. ULIONDOKA KAMA MASIHARA SHANGAZI YANGU, ULIONDOKA NIKIWA BADO NAHITAJI UWEPO WAKO MTOTO WANGU. KAZI YA MUNGU SIWEZI KUIZUNGUMZIA SANA. NILIKUPENDA SANA NIA WANGU, NAKUPENDA SANA NIA, NA NTAKUPENDA MILELE MY LOVE. HAKUNA SIKU INAYOPITA BILA KUTAJA JINA LAKO AU KITUKO CHAKO MAMA YANGU. SIJUI NIELEZEJE MAUMIVU NILIYONAYO SAA HIZI NIANDIKAPO HILI. AAAAAAAH SANIA WANGU, NYOTA YANGU, KIPENZI CHANGU. MMMMMH HAYA NAHISI SINA LA ZIADA ZAIDI YA HILO. LALA SALAMA KIPENZI CHANGU. UMEONDOKA MAPEMA SANA. UMEONDOKA NIKIWA NDO KWANZA NAANZA KUONA RAHA YA UWEPO WAKO MAANA ULIKUWA UNAJUA KUPENDWA NA KUDEKA KWA AKUPENDAE. LALA SALAMA NIA.
PICHA INAYONITOA MACHOZI KILA NINAPOITAZAMA
NAIKUMBUKA PICHA HII, ULINIMBIA AUNTY NGOJA NIKUWEKEE POZI, NAKUMBUKA KUIITA POZI LA JUMAPILI, SANIA NAKOSA VINGI KUTOKA KWAKO
HAPA NILIKUWA NAAMBIWA BAYAAAA, NAKUMBUKA TULIKUWA HOSPITALI NDO ULIKUWA UMEANZA KUUMWA SHANGAZI YANGU
Friday, 18 September 2015
BADO TUTAENDELEA KUSIKIA NA KUONA MENGI. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Makamu Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi, Laeticia Ghati Musore, akizungumza juu ya ukiukaji wa taratibu katika Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA katika Hoteli ya Land Mark Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI, Mosena Nyambabe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatima yao ya kupambana kama wenyewe
UTANGULIZI
Sisi viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu tukiwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa na viongozi wengine, tumekuja mbele yenu mtusaidie kufikisha ujumbe maalum kwa wanachama wetu na Watanzania wote wanaokiamini chama chetu,
Tumefika kuelezea kutoridhishwa na mwenendo wa ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA. Tumekuja pia kuwaelezea ni hatua gani tulizoamua kuchukua kukabiliana na changamoto hii.
Wengi wenu mnafahamu kuwa UKAWA ni Umoja wa Katiba ya Wananchi ulionzishwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba kutetea Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi dhidi ya uchakachuaji uliokuwa unafanywa na CCM.
UKAWA siyo chama cha siasa bali umoja. NCCR-Mageuzi iliamua kujiunga na harakati hizi kwa nia njema ya kutetea maslahi ya taifa letu. Zaidi ya mwaka sasa tangu tujiunge na umoja huu, matokeo yake yamekuwa ni mabaya kwa uhai na ustawi wa chama chetu. Wakati vyama vingine vimezidi kuimarika ndani ya UKAWA, NCCR-Mageuzi imedhoofika. Hali hii haikubaliki.
MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO BAINA YA VYAMA VYA UKAWA
Vyama vinavyounda UKAWA, vilisaini Makubaliano ya Ushirikiano katika Mkutano wa Hadhara kwenye viwanja vya Jangwani. Kitendo hicho kiliwavutia na kuwapa matumaini wananchi na wao wakazidi kutuunga mkono. Iliamuliwa kwamba tusiuwe vyama vyetu bali tuunganishe nguvu za vyama vyetu kama namna ya kujiimarisha kwa pamoja.
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA DISEMBA 2014.
Kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014, vyama vinavyounda UKAWA vilitiliana saini ya Mwongozo wa Ushirikiano katika Uchaguzi huo.
Licha ya kutiliana saini Makubaliano hayo, bado kulikuwa na ukiukwaji mkubwa na wa makusudi wa Mwongozo huo.
Licha ya kuzijadili changamoto zilizojitokeza katika Uchaguzi huo, lakini hazikupatiwa ufumbuzi wowote.
Sisi tuliopo hapa tulionya mapema kuhusu mwenendo huu wa kuvunja makubaliano na tukaomba taratibu tulizokubaliana zitumike ili kurudi kwenye misingi ya UKAWA lakini hatukusikilizwa.
USHIRIKIANO KATIKA UCHAGUZI MKUU, OKTOBA 2015.
Licha ya changamoto zilizokuwepo, tuliamua kwa pamoja kwamba vyama vya UKAWA tuingie katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na makubaliano ya ushirikiano, ikiwemo kuwa na mgombea mmoja wa Urais na kuachiana majimbo ya uchaguzi.
Pia, katika kuendesha umoja huu, tuliunda vyombo vya kutusaidia ambavyo ni:-
- Kamati ya Wenyeviti.
- Kamati ya Makatibu Wakuu.
- Kamati ya Ufundi.
- Kamati ya Wataalam.
Pamoja na kuunda vyombo vya kuendesha UKAWA, tangu Januari 2015, bado tumeshindwa kujenga UKAWA imara na tuliyotarajia kwa manufaa ya wanaukawa na wananchi kwa ujumla.
Yafuatayo yamethibitisha hili jambo:
- Tumeshindwa kuweka Kanuni za uendeshaji wa UKAWA kama tulivyokubaliana. Kwa maana hiyo,tunafanya mambo kiholela
- Tumeshindwa kuunda Kamati zitakazoshughulikia migogoro baina ya vyama.
- Tumeshindwa kuunda na kuzisimamia Kamati za Majimbo
- Tumeshindwa kupata muafaka wa kuachiana majimbo.
Mfano, NCCR – Mageuzi tuliachiwa majimbo 12 ya Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini, Muhambwe, Kasulu Mjini, Vunjo, Ileje, Mbinga Mjini, Manyovu, Buyungu, Ngara, Nkenge na Korogwe mjini. Ikumbukwe kwamba, mwaka 2010, NCCR-Mageuzi ilisimamisha wagombea katika majimbo 67.
Kwa maana hiyo, UKAWA umeturidisha nyuma katika kupata wabunge na kuimarisha chama zaidi ya miaka 20 baada ya kuundwa kwake.
Licha ya kukubaliana kwamba NCCR-Mageuzi iachiwe majimbo 12, wenzetu wa vyama vingine katika UKAWA wamesimamisha wagombea katika majimbo 6 kati ya hayo. Wametuvunja moyo na kutuonyesha kwamba hawatujali. Na hata kule ambapo katika majimbo sita ambapo wametuachia bado wenzetu wanatufanyia fujo kuliko hata wanazotufanyia wanachama wa CCM. Tunamifano mingi ya kuonyesha ni jinsi gani wagombea wetu wanavyofanyiwa vurugu.
- Tumeshindwa kupata muafaka wa namna ya kuachiana wagombea udiwani katika kata nyingi.
- Tumeshindwa kuonesha na kukubaliana kila chama kitapata nafasi gani na ngapi katika Serikali ya UKAWA.
- Tumeshindwa kufuata utaratibu wa kumpata mgombea Urais wa UKAWA
- Tumeshuhudia vurugu kubwa iliyoletwa ndani ya UKAWA na wanachama waliotoka CCM na wao kupewa umuhimu kuliko viongozi wa UKAWA. Zaidi ya Mbatia hakuna kiongozi wa NCCR-Mageuzi anayeshirikishwa, anayezungumza au aliyepo kwenye kampeni za mgombea Urais wa UKAWA.
- Tumeshindwa kuwa na timu ya kampeni timu ya UKAWA, ambayo inagharamiwa na UKAWA na inatafuta fedha pamoja, kama ilivyokubaliwa.
- Tunashuhudia UKAWA ambayo Chadema ndiyo UKAWA-Bara na CUF ndio UKAWA-Zanzibar. Chadema haijali Zanzibar na CUF haijali Bara. Na NCCR-Mageuzi haipo huku wala kule ikiendelea kudhoofika siku hadi siku.
- Tumeshindwa kuona uwazi katika matumizi ya fedha na maamuzi muhimu ya uendeshaji wa UKAWA.
- Tumefadhaishwa na kuvunjwa kwa misingi ya kuanzisha kwa UKAWA.
- Wakati NCCR imetii mgawanyo wa majimbo kwa vyama vinavyounda UKAWA, vyama vingine na hasa CHADEMA vimesimamisha wagombea kinyume cha makubaliano.
NINI KIFANYIKE NA UKAWA
Hatukuwaita hapa kuwaambia kwamba tunajiuzulu siasa kutokana na changamoto hizi. Tumeamua kupambana na kurudisha hadhi na heshima ya Chama chetu. Hatuwezi kubwaga manyanga. Tunataka kuitoa CCM madarakani kutokana na ulaghai na ujanja-ujanja wa miaka 50. Lakini hatuwezi kuitoa CCM kwa mbinu za ulaghai na ujanja-ujanja. Tunakwenda kukabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi na Watanzania. Tunao wajibu wa kujiongoza vizuri ili tuwaonyeshe Watanzania kwamba tuna uwezo wa kuwaongoza vizuri.
WITO WETU
- Tunamshauri Mwenyekiti wetu, ndg. James Mbatia, aitishe vikao vya kikatiba ili tuweze kujadiliana kuhusu hatima ya chama chetu.
- Tunashauri ndg. Mbatia asiwemsemaji wa CHADEMA wakati anakiacha chama chake (NCCR-Mageuzi) kinadhoofika. Kwa mfano, Dr. Slaa alipoishambulia Chadema hakuna kiongozi wa Chadema aliyemjibu isipokuwa Mbatia ndiye aliyeamua kujiingiza kwenye ugomvi ndani ya Chadema.
- Tutachangishana ili tusafiri kwenye majimbo na kata za wagombea wetu na kuwasaidia kwenye kampeni ili wasibaki wapweke kama yatima.
- Tunasisitiza kwamba upinzani wa kweli nchini hauwezi kujengwa kwa njia za hila, kwa kukiuka taratibu za kidemokrasia tulizojiwekea wenyewe, kwa kukiuka misingi muhimu kama uadilifu, kwa kuweka mbele tamaa na maslahi binafsi kuliko taifa, kwa kutegemea propaganda. Tukifanya hivi, wananchi watashindwa kututoufautisha na CCM na wataamua kuchagua zimwi walijualo. Hatari hii tunaiona wazi kabisa.
……………………………
Leticia Ghati Mossore
Makamu Mwenyekiti (Bara)
NCCR-Mageuzi
17.09.2015
Mosena Nyambabe
Katibu Mkuu, NCCR Mageuzi
Wednesday, 16 September 2015
Tuesday, 15 September 2015
MAMBO YANAZIDI KUWA MAMBO,MBONA TUTASIKIA MENGI
"Nimeamua kuondoka Chadema na vuguvugu la Ukawa kwa sababu mbalimbali: moja ni ubovu wa kimfumo katika uongozi, uratibu na misimamo. Fujo: Wafuasi wengi Ukawa bado wana muhemko kwenye kufanya mambo. Naamini uongozi wa nchi unahitaji busara kuhimili kazi. Tumefeli hilo. Kwa siku 39 zilizobaki nitaongea na mamilioni ya mashabiki wangu kuhusu msimamo wangu. Naondoka Chadema, nitamuunga mkono Magufuli". Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika Aunt Ezekiel
Monday, 14 September 2015
Friday, 11 September 2015
Thursday, 10 September 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)