Bondia Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12 la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katika raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini, jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na kisha kuendelea na pambano.
Baada ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa na madhara kwa Cheka.Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi.
Cheka, alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo na kushambuliwa mfululizo. Na Mafoto Blog.
Cheka akitangazwa mshindi kwa pointi na mwamuzi kutoka chama cha ngumi WBF....
Cheka akishangilia ushindi wake.....
Mashabiki wakimbeba cheka kwa furaha.......
Cheka akivishwa mkanda wa ubingwa.....baada ya kutangazwa mshindi....
Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake....
Cheka akijibu mapigo....
pambano likiendelea....
Wakiliana taimingi.....
Mimi sijui hapa Cheka alikuwa akifanya kitu gani sijui alikuwa akikwepa konde ama akijihami kwa kutoka nduki....
Muda wote Mserbia alionekana kujihami kwa staili hii.....
Cheka akitupiamo ......
Hapa sasa hata mimi sijui ilikuwa ni kitu gani kwamba ni konde zito, mieleka ama nini.....
Cheka sijui alikuwa akifanya nini hapa....
Mserbia akitupiamo....
Mwamuzi akimhesabia Cheka baada ya kuanguka katika raundi ya kwanza.....