Monday, 25 February 2013

SHUKRANI WAPENDWA WANGU WOTE


NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WOTE WALIOFANIKISHA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KUMALIZA MSIBA WA MAMA YANGU KIPENZI BIBI TABU C. MAHIMBALI. SINA NENO SAHIHI NINALOWEZA KUSEMA ZAIDI YA ASANTE NA MUNGU AWAJAALIE KILA LILILO LA KHERI. SIWEZI KUWATAJA WOTE KWA MAJINA ILA NINACHOWEZA KUSEMA KUWA ASANTENI SANA KWA UPENDO MLIOUONYESHA KWETU SOTE. MIMI NA FAMILIA YANGU TUTAKUWA WATOVU WA NIDHAMU KAMA HATUTASEMA NENO ASANTE SANA. NAMSHUKURU MUNGU PIA KWA KUSIMAMIA KILA KITU KIENDE SALAMA KAMA KILIVYOPANGWA. ASANTENI SANA.



KAKA AKIREKEBISHA BAADA YA KUPANDA SHAHIDI KABURINI



MZUWANDA WA MAMA, BABA NA SHEIKH SAID WAKIANGALIA

ZOEZI HILI LA KUVUSHA WATOTO LILIFANYIKA MARA MBILI HALAFU SIKUELEWA KWA NINI. MNISAIDIE




MY WII ROSE AKIREKEBISHA UDONGO BAADA YA KUWEKA SHAHIDI.

BABA WA PILIL KUTOKA KULIA, HII ILIKUWA SIKU YA KUZIKA

KAKA MKUBWA ANDREW MWENYE SHATI YA KITENGE SIKU YA MSIBA

MDOGO WANGU ANAYENIFUATIA KUZALIWA JACOB

MISS YOU MUM, WISH YOU WERE HERE


I MISS THIS SMILE A LOT


BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Friday, 15 February 2013

IJUMAA KAREEM

ALLAHUMMA KWA REHMA ZAKO, TUNAKUOMBA USIUKUNJE UKURASA WA SIKU HII YA LEO. ILA
 "UMESHASITIRI MABAYA YETU"
"UMESHAFUTA MAOVU YETU"
"UMESHAKUBALI TOUBA ZETU"
UMESHAJIBU DUA ZETU"
YARABI IJAALIE IJUMAA HII IWE  YENYE KHERI KWETU NA KWA KILA TUWAPENDAO. TUJAALIE JANNA PAMOJA NA WAZEE WETU WALIOTANGULIA.








Thursday, 14 February 2013

HAPPY VALENTINE'S DAY MAMA



 MAMA, LEO NI SIKU YA 30 TOKA ULIPOZIKWA NA SIKU YA 32 TOKA ULIPOFARIKI DUNIA. ZIMEKUWA SIKU NGUMU NA ZA MACHUNGU KATIKA MAISHA YANGU. SIJAWAHI KUWA NA SIKU NGUMU KAMA HIZI TOKA ULIPONILETA DUNIANI. NIMESHATAMANI MARA NYINGI JAPO KUONGEA NA WEWE AU KUKUPIGIA SIMU ILI MRADI NISIKIE JAPO SAUTI YAKO. NIMESHAWAHI KUPIGA SIMU YAKO PIA AMBAYO IKAITIA KWENYE POCHI YANGU MWENYEWE NA KUBAKI NIMETOA MACHO TU. JUST IMAGINE SIMU NIMEPIGA MWENYEWE NA BADO NIKAINGIZA MKONO KWENYE POCHI KUTOA SIMU KUONA NANI ANAPIGA. NIKAKUTANA NA JINA LANGU MWENYEWE “FAIDA MY MUM MORO” HOW ROMANTIC. HALI HII IMEJIRUDIA TENA LEO, IKIWA SIKU YA WAPENDANAO TUMEKUWA NA KAWAIDA YA KUCHAT SIKU NZIMA LABDA KWA SMS AU KUPIGIANA SIMU. MAMA, NATAMANI KUSIKIA SAUTI YAKO NA KUPATA YALE MANENO YAKO MATAMU YA UPENDO ULIYOZOEA KUNIPA. MAMA, SIJAWAHI KUCHEKA KAMA NILIVYOZOEA KUCHEKA NA WEWE TOKA ULIPOENDA. MAMA, WHERE ARE YOU?? HOW MANY TIMES DO YOU WANT ME TO CALL YOU?? SAWA, HUTAKI KUITIKA BASI NIAMBIE NAISHIJE BILA WEWE?? NIAMBIE NIANZIE WAPI HALAFU UKAE KIMYA TENA. NIMEJITAHIDI SANA KUSIMAMA MWENYEWE KATIKA SIKU HIZI 30/32 BILA MAFANIKIO. NIMEJITAHIDI SANA KUWA MAMA KWA ANNA NAHISI KUFELI. NIAMBIE SIRI YAKO YA KUWA MAMA BORA KWETU. ULIKUWA NA KAWAIDA YA KUNIAMBIA YOTE KWANINI HILI ULINIFICHA?? AU ULITAKA NIFUMBUE MWENYEWE? UJUE LIMEKUWA FUMBO GUMU SANA MAMA NA LINAUMA KUONA KUWA NAFELI MAHALI AMBAPO KUNA MTU ANATARAJIA NITAFAULU. NISAIDIE MAMA KUJUA HILI, NIMEKWAMA. UNAJUA ANNA ALINIAMBIA NINI SIKU ULIPOFARIKI?? ALINIAMBIA DADA WEWE SASA UNAKUWA MAMA YANGU, MAMA KATUACHA WENYEWE. MAMA, MPAKA LEO NINAPOANDIKA HAYA NI KWAMBA NIMESHINDWA KUWA MAMA KWA ANNA. NIMESHINDWA KUTIMIZA NILICHOMUAHIDI KUWA NITAKUWA MAMA KAMA WEWE. NIAMBIE BASI MAMA NIFANYEJE ILI NIWE JAPO ROBO YA WEWE, NIAMBIE NIFANYE NINI ILI NIWEZE KUMFANYA ANNA AENDELEE KUWA ALIVYOKUWA?? EEEEH MUNGU NIONYESHE NJIA MIMI, SITAKI KUKUKUFURU MUNGU WANGU ILA NAUMIA SANA. MPE WEPESI KIPENZI CHANGU, MPUNGUZIE ADHABU YA KABURI MAMA YANGU NA UMPE PEPO YAKO ILA SI KWA MAPENZI YANGU ILA UPENDAVYO WEWE MUNGU WANGU. ANNA WANGU, TAFADHALI MAMA YANGU ENDELEA KUNIVUMILIA, NINA HAKIKA SIKU MOJA NITAFANYA SAWA TU. NAJITAHIDI KUMUOMBA MUNGU SANA ILI NIFANYE KILE KITAKACHOLETA ILE FURAHA YAKO ULIYOKUWA NAYO MWANZO. NISAIDIE KUNIKUMBUSHA PALE NITAKAPOENDA NJE NA UYAPENDAYO. NAKUPENDA SANA DADA. MUNGU WANGU MTIE NGUVU BABA YANGU MPENZI, NI DIAMOND PEKEE NILIYOBAKI NAYO KWA SASA. MUONGEZEE SIKU ZA KUISHI ILI AENDELEE KUSIMAMA KATI YETU KAMA MAMA ALIVYOKUWA. NAKUPENDA SANA BABA YANGU. MISS YOU MAMA NA NAKUPENDA SANA MAMA YANGU. HAPPY VALENTINE MAMA.

LOVE YOU MUM, MISS YOU MUM, HAPPY VALENTINE'S DAY MAMA

Monday, 11 February 2013

REST IN PEACE EVA

TAREHE 08/02/2013 TUMEPOTEZA MFANYAKAZI MWENZETU, DADA EVA GEORGE. NILIPATA KUFANYA KAZI NA HUYU DADA KWA MIAKA MITANO NA AKAWA MTIIFU KWANGU KUPITA MAELEZO. ALIKUWA ZAIDI YA MDOGO WANGU KAMA SIO MY BEST WORK MATE. ALIKUWA TAYARI KUFANYA CHOCHOTE UTAKACHOMUAGIZA BILA MALALAMIKO. EEE MWENYEZI MUNGU MPE PUMZIKO LA MILELE DADA EVA GEORGE NADOO. 

HAPA AKIWA KAZINI

POPOTE NILIPOKUWA NAKWENDA NILIKUWA NAYE, HAPA TUKIWA HOSPITALI AMNISINDIKIZA NIKIWA NAUMWA

SHE WAS BEATIFUL

WAKATI WOTE TULIKUWA KAMA KUMBIKUMBI.

WHAT A SMILE

EVA, GONE TOO SOON



MY DEAR, MISS YOU MUCH ALREADY
BAADA YA KUTOKA KUZIKA

WACHACHE TULIOJAALIWA KWENDA KUZIKA KIJIJINI KWAO GAIRO, TULIMUACHA EVA MITA CHACHE KUTOKA TULIKOSIMAMA


NILIVUTIWA NA HII NYUMBA TU JAMANI.




Wednesday, 6 February 2013

I MISS YOU SO VERY MUCH

Looking back on everything,
I still remember her smile.
I wish things didn't end so soon,
And turn back time for awhile.

No matter how much it hurts,
I still love her so.
A part of me needs her so much,
Can't seem to let her go.

Knowing I won't be able to see her,
Makes my heart cry out in pain.
I can't believe we won't talk anymore,
The thought makes me wanna go insane.

She was my reason for waking up,
For the smile you see on my face.
Going a single day without her,
Makes me feel so out of place.

I was afraid of opening up,
Now I'm afraid of the next day.
Whenever I see her one last time,
I'm terrified of what she may say.

But when I see her one last time,
I won't know what to do...
When she tells me that last goodbye,
I'll whisper,"I already miss you.."
 
LOVE YOU MUCH MUM.


 





Friday, 1 February 2013

MOROGORO YETU ASUBUHI HII

KUMENYESHA MVUA KUBWA SANA LEO SAA 12 ASUBUHI, NIKATOKA ILI NIONE NINI KINAENDELEA, NIKAKUTANA NA HIKI. SAMAHANI PICHA HAZIKO VIZURI KUTOKANA NA HALI YA HEWA
NAHISI WAKATI NAPIGA PICHA NILIKUTANA NA RADI, ILA NIMEIPENDA

HAYA NI MAENEO YA KIHONDA


MAJI YALIKUWA YANAKIMBIZANA VIBAYA MPAKA NIKAOGOPA KUSOGELEA



HUU NI MFEREJI ULIOPO NJE YA NYUMBA YETU, UMEFURIKA MBAYA




HUU NI MFEREJI ULIOPO NJE YA NYUMBA YETU, UMEFURIKA MBAYA

ILA MANDHARI INAVUTIA HADI RAHA




KWA SABABU YA KUPIGA PICHA MPAKA TUKAACHWA NA GARI YA KAZINI


MGONJWA WA BARIDI KAMA KAWAIDA YAKE, NA BLANKETI BARABARANI


PUNGUZA UMBEYA KHAAAAAAAA

ONA ALIVYOJIKUNYATA KAMA KUKU MWENYE MDONDO

HAPO SAWA UMEJIACHIA MPAKA UMEPENDEZA

TUKIWA KITUONI TUNASUBIRI GARI



WACHA WEEE, I LOVE THIS PICTURE

KWENYE GARI KUELEKEA KAZINI, NAYO SAFARI UJUE KM15 KILA SIKU!!


MAENEO YA MSAMVU



MAENEO YA NANENANE



OFISINI TAYARI