Friday 22 March 2013

KUMBUKUMBU

MOHAMED NAHAMA

IMETIMIA MIAKA MITANO LEO TOKA ULIPOFARIKI DUNIA TAREHE 22/03/2008. IMEKUWA MIAKA MITANO AMBAYO HAIJAWAHI KUPITA SIKU BILA KUKUMBUKA UWEPO WAKO. NAHISI NIMEPUNGUA KILA KITU BILA WEWE MPENZI WANGU, ULIKUWA KILA KITU KWANGU NA SIJUI KAMA NITAWEZA ZAIDI YA ULIPONIFIKISHA WEWE. SIJUI KAMA KUNA LA ZIADA LA KUONGEA AU KUANDIKA ILI KUJUA JINSI NILIVYOKUKOSA KATIKA MAISHA YANGU. MUDDY, ULINIONGOZA MAHALI AMBAPO SIJUI KAMA KUNA ATAKAYEWEZA KUNIONGOZA KWA SASA. ULIKUWA ZAIDI YA MWALIMU KATIKA MAISHA YANGU YA KILA SIKU KAMA MUME. NAOGOPA KUONGEA MENGI MAANA NAHISI NINAKOELEKEA NAENDA KUMKUFURU MUNGU WANGU NA MIMI SITAKI HILO LITOKEE. NINACHOWEZA KUSEMA KUWA, MUNGU AKUPE RAHA YA MILELE NA MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE UPUMZIKE KWA AMANI, AMINA. NILIKUPENDA, NAKUPENDA NA NITAENDELEA KUKUPENDA MPAKA MUNGU ATAKAPONIITA MBELE ZA HAKI YAKE ILI TUUNGANE TENA KATIKA UFALME WAKE.

ULIKUWA FURAHA YANGU KILA TULIPOENDA

TULIKUWA TUNAFANANA KWA KILA KITU AKILI, TABIA NA HATA VITUKO. NA KAMA TULITOFAUTIANA BASI NI PADOGO SANA

BAUNSA WANGU, WEWE NDIE PEKEE ULIYENIFUNDISHA KURUSHA NGUMI KAMA MWANAUME.

MY SWEETPIE, MISSING YOU A LOT BABY.

No comments: