HII NDO HALI HALISI LEO HII HUKU KWETU MOROGORO BAADA YA MABASI MADOGO YA ABIRIA MAARUFU KAMA DALADALA KUGOMA. CHANZO CHA MGOMO HUO AMBAO WENYEWE WANASEMA HAWAJAGOMA ILA WAMESITISHA HUDUMA HIYO KWA MUDA NI UGOMVI WAO NA ASKARI WA BARABARANI AMBAO WAMEKUWA WAKIWAKAMATA BILA MPANGILIO MAALUM NA KUWATOZA TOZO KUBWA TOFAUTI NA UTAFUTAJI WAO WA SIKU. MGOMO HUO UNAWEZA KWISHA IWAPO MAASKARI HAO WATAKUBALI KUKAA MEZA MOJA NA WAMILIKI WA MAGARI HAYO. TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA NINI KINAENDELEA.
No comments:
Post a Comment