Monday, 12 January 2015

R.I.P MAMA. IMETIMIA MIAKA MIWILI LEO MAMA. MISS YOU AND LOVE YOU ALWAYS




MAMA, IMETIMIA MIAKA MIWILI SASA TOKA ULIPOFARIKI NA KUTUACHA WENYEWE. NI MIAKA MIWILI YENYE UGUMU USIOMITHILIKA KWETU MAMA, UKWELI UTABAKI PALEPALE KWAMBA WEWE NDO ULIKUWA BAUNSA WETU. NAANDIKA HIVI KAMA MASIHARA LAKINI NAMAANISHA KILA HERUFI. UGUMU TUNAOPITIA SASA NADHANI UNGEKUWEPO HALI INGEKUWA TOFAUTI. HAKUNA SIKU KATIKA MAISHA YANGU TOKA ULIPOENDA INAISHA BILA KUKUTIA MDOMONI EIDHA KWA SAUTI AU KIMYA KIMYA. MUNGU MWENYEWE NDO ANAJUA HALI NILIYONAYO TOKA ULIPOFARIKI. KUNA WAKATI HUWA NAKUFURU MUNGU NA KUTAMANI ULIPO. HASA SASA MAMA, NIPO KWENYE KIPINDI KIGUMU SANA MAMA YANGU, KWA NINI ILIKUWA UENDE?? NAJUA NI LAZIMA UENDE ILA ILIKUWA MAPEMA SANA MAMA. NAKUMBUKA MENGI KUTOKA KWAKO ILA KWA SASA NAKUMBUKA MANENO ULIYOWAHI KUSEMA KUWA "NIKIFA MTAPATA SHIDA SANA" NA NDICHO KINACHOTOKEA KWA UPANDE WANGU. NAJUA MUNGU ANAJUA MAUMIVU NILIYONAYO MWILINI NA MOYONI NA MALAIKA PIA WANAKULETEA MATESO YANGU. SIMAMA NA MIMI MAMA KAMA ULIVYOZOEA KUSIMAMA MAMA. NATESEKA PEKE YANGU MAMA. NAJUA NAANDIKA MENGI AMBAYO SIKUTAKIWA KUANDIKA ILA NAFANYA HIVI LABDA UCHUNGU NILIONAO UTAPUNGUA. NAKUTAMANI POPOTE ULIPO MAMA. SEMA NAMI JAPO KIDOGO MAMA ILI TUFUNGUE HILI LILILOPO. MAISHA YANGU YAMEKUWA KAMA MASIHARA MPENZI WANGU. MISS YOU VERY MUCH MAMA AND I WISH YOU WERE HERE NOW.

MISS YOU MAMA

ALWAYS HAPPY, I MISS EVERYTHING FROM YOU MAMA

LALA SALAMA MAMA YANGU NA MUNGU AKUPUNGUZIE ADHABU YA KABURI. NAKUPENDA SANA MAMA

No comments: