Mama, inapofika kipindi kama hiki tunachopitia katika familia, huwa nautamani uwepo wako. Mama tupo kwenye wakati mgumu na unajua mama. Nimejitahidi kulichulia poa toka jana nilipolipata nahisi kushindwa mama. Please mum pigana na sisi, simama na sisi bado tunahitaji msaada wako kwa nguvu zote. Unakumbuka uliwahi kusema kuwa utafanya lolote hata liwe gumu kiasi gani kwa ajili ya watoto wako?? Wakati wa kufanya lolote umefika mama, najua yote yasingetokea kama ungekuwepo, na hata kama yangetokea si kwa kiasi kikubwa.Eeee Mungu tuhurumie baba maana tumechoka kulia. Tusimamie baba.
Samahani kwa kuliweka hili hapa ila nahisi labda moyo wangu utafunguka japo kidogo maana nimekabwa mpaka nahisi kushindwa kuongea. Mama tusaidie kurejesha furaha yetu mama. MISS YOU MUCH MAMA KATIBU AND LOVE YOU ALWAYS. R.I.P MUM
No comments:
Post a Comment