Wednesday 23 January 2013

REST IN PEACE MAMA




Sijui nianzie wapi, Kwangu mimi ni mpiganaji wa hali ya juu, alikuwa zaidi ya mama, rafiki yangu, shoga yangu, msiri wangu, mshauri wangu na mpiganaji wangu (greatest mother in the world). Mama yangu ndio alikuwa kila kitu kwangu. Hakuna nililokuwa naweza kufanya bila yeye, hapa nilipo nisingefika bila yeye. nashindwa kupata neno sahihi la kuandika au kuelezea wasifu wa mwanamke huyu. Nimepoteza lulu katika maisha yangu, nimepoteza ngao muhimu na mhimili mkuu katika maisha yangu. Natamani japo angerudi au nimuone tena ili tuweze kufanya yale tuliyozoea kufanya. Tucheke pamoja, tupike pamoja au tulie pamoja wakati mwingine. Mama, nitawezaje bila wewe? Nitafanye bila wewe? Nianzie wapi mama? nifanye nini mimi mama? ulikuwa unajibu maswali yote haya ila sasa sina wa kunijibu maswali yangu, sina wa kufanya ya kwangu maana ulikuwa unafanya kila kitu. Tarehe 12/01/2013 ilikuwa siku ngumu sana kwangu, sikuamini kilichotokea na bado siamini. Wakati mwingine huwa nahisi nipo kwenye ndoto ndefu na ya kutisha ambapo itaisha nitaamka na kukupigia simu mama yangu na uanze kuleta utani wako wa kila siku ambao unanifanya nicheke mpaka walio karibu wanione labda nachanganyikiwa. Eeeeh Mungu nitie nguvu mimi na familia yangu hasa mdogo wangu mpenzi Anna ambaye mama alikuwa kama roho yake, nitafanya nini na Anna mimi, nitaanzia wapi na Anna mimi? Mama huu ni mtihani mwingine ulioutupa kwenye mikono yangu. Umeniachia ya kwangu lakini bado umeniachia ya Anna pia. Bado nahitaji msaada wako mama peke yangu siwezi. Namuomba Mungu anijaalie subra na anipe wepesi kwa kila jambo. Najua bado upo pamoja nasi kama ulivyokuwa ingawa kwa sasa itakuwa tofauti. Mama yangu, nyota yangu, nguzo yangu, kipenzi cha roho yangu, kama nilivyokuheshimu wakati wa uhai wako sitaacha kufanya hivyo milele. Kama nilivyokupenda kipindi cha uhai wako sitaacha kufanya hivyo daima. Nilikupenda, nakupenda na nitakupenda milele mpaka mwisho wa maisha yangu tutakapokutana tena. Naomba Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi na akulaze mahali pema peponi kipenzi changu, aaamen.


 

My super woman and Anna

Mum, Anna & Dad hii ilikuwa November 2012

6 comments:

Anonymous said...

Pole dada yangu ila mwisho wa siku inatubidi tukubali matokeo na naamini mama yupo pamoja nawe najua atakusaidia kuendelea kunilea vyema dada yangu. Mungu yupo nasi tutaweza tu dada yangu... punguza kulia na kuwaza sana anajua unaweza hivyo kaenda kwa amani akijua utanilea.... luv u so much my sister and new Mother. REST IN PEACE MAMA NA BIBI

Winnie Ngalaba said...

Asante sana dada yangu mpenzi, NAHITAJI ZAIDI MSAADA KUTOKA KWAKO MAMA, KUKAA KIMYA NA KULIA HAKUTAFANYA NIJUE NINI UNATAKA AU NINI UNAPENDA. NISAIDIE MDOGO WANGU ILI TUWEZE KUFANYA YALE MAMA ALIYOPENDA TUFANYE. NAKUPENDA SANA MY LIL SIS

Anonymous said...

poleni sana my 2wi ,ni msiba wetu wote inna lillah wainna ilaihi rajiuna

Anonymous said...

mola ailaze roho ya mpenzi mama yetu peponi,aaameen,wadogo zangu winnie ,YAKUBU NA ANNA tuwe wavumilivu kaka fundi

Winnie Ngalaba said...

kweli kabisa wi, ni msiba wetu sote na tushukuru mola kwa kila jambo.

Winnie Ngalaba said...

inshaallah kaka yangu, Mola pekee ndiye atakayeweza kutupa huo uvumilivu. tumuombe ili atupe na subra pia