Thursday 18 June 2015

HIVI INAKUWAJE MAMA MZAZI UNASHIRIKI UKATILI HUU KWA MWANAO WA KUMZAA?? AKILI AU MATOPE??

Credit: Dustan Shekidele

UKATILI ULIOJE! WAZAZI WAMPIGA, WAMFUNGA KAMBA MTOTO WAO, WAMFUNGIA NDANI
 Bi,Asha Mohamed ambaye ni mama mzazi wa mtoto Salum akihojiwa na mwandis
hi wa Mtandao huu nje ya nyumba yake iliyopo maeneo ya Mkundi  huku  kufuli kubwa likining'inia kwenye chumba alichomfungia mwanae wa kumzaa kwa kushirikiana na baba wa kambo wa mtoto huyo.

 Polisi walifika eneo la tukio na kumhoji mama huyo.
              .....Akihojiwa na mwandishi wa habari  huku akirekodiwa
 Mdogo wa Salumu akizungumza jinsi alivyoshuhudia kaka yake alivyoteswa usiku kucha na wazazi wake
 Katika hali ya kushangaza mwanaume huyo aliayefahamika kwa jina moja la Ally baada ya kuwaona Polisi na waandishi wa habari alikimbia na fungu ya mlango jambo lililowaradhimu polisi kuamulu mlango huo kuvunjwa na kuokoa maisha ya mtoto Salum
 Baada ya mlango kuvunjwa polisi na mwandishi wa habari hizi waliingia ndani na kumshuhudia mtoto Salum akiwa ndani ya chandarua  akifungwa miguu na mikono kwa nyuma



              Polisi wakimfungua kamba

 Polisi pamoja na mwandishi wa Mtandao huu wakifanya mahojiano na mtoto huyo baada ya kufunguliwa kamba.
 Mtoto ayuko akitolewa nje na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano zaidi


 Polisi wakimuokoa mama wa mtoto huyo akipokee mkong'otoa kitoka kwa majirani zake waliokuwa na hasira
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Katika hali inayoonyesha ukatili wa ajabu, mwanamke mmoja aliyejulikana  kwa jina la  Asha Mohamed, akishirikiana na mumewe, walimfunga kamba miguu na mikono mwanaye wa kumzaa Salum Mohamed (9) na kumfungia ndani ya nyumba yake huku wenyewe wakienda kusikojulikana muda mrefu Jumatatu iliyopita huko Mkundi, nje kidogo ya mji wa Morogoro.
 Tukio hilo la kusikitisha lilifanyika ikiwa ni adhabu ya mtoto huyo kutokana kosa la kuchana chandarua kwa miguu, kitendo alichokifanya usiku wa Jumapili, ambako licha ya kupigwa kwa zaidi ya saa mbili mfululizo, pia alinyimwa chakula na hivyo kulala na njaa.
Kwa mujibu wa majirani Mwanamke huyo na mumewe kwa muda mrefu walikuwa wakimfanyia vitendo vya kikatili mtoto huyo”kuna wakati mtoto huyu aliamua kutembea kwa kwa miguu kutoka hapa mkundi mpaka mjini kwa bibi yake umbali wa kilomita 10.
“Wazazi wake jana majira ya saa 3 mpaka saa 5 usiku walimpiga sana huyu mtoto, cha ajabu asubuhi walimfunga kamba na kumfungia kwa nje na kufuli kubwa na wenyewe kwenda kwenye shughuli zao, alishindwa kwenda shule, tulipomuuliza kupitia dirishani, alisema alipewa adhabu hiyo baada ya kuchana chandarua, kwa uchungu tukaamua kutoa taarifa kwako,
” alisema Mage Luzimamu, mmoja wa majirani.
Baada ya mwandishi kupata taarifa hizo aliwasiliana na Jeshi la Polisi ambapo askari walienda hadi ilipo nyumba hiyo na kulazimika kuvunja mlango na baadaye kumfungua mtoto huyo na kuondoka naye. Mama mzazi alipatikana na kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alijitetea kuwa alimfunga kamba kama sehemu ya adhabu na siyo mateso.
Mume wa mama huyo alikimbia baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake lakini Polisi wamesema watamtafuta hadi wamtie mbaroni.

No comments: