SAMAHANI KAMA NIMEANZA VIBAYA, JANA WAKATI NAANGALIA TAARIFA YA HABARI YA ITV NIKAKUTANA NA TAARIFA INAYOZUNGUMZIA BAADHI YA WATU KUSHIKILIA LINE ZA MAENEO NYETI. NINAPOZUNGUMZIA MAENEO NYETI NAMAANISHA POLISI, FIRE NA KWINGINEKO. MTU ANAPIGA SIMU FIRE NA KUOMBA AAMBIWE NINI AFANYE KWA KUWA SIMU YAKE INAKOROMA HIVI NI KWELI AU UTANI? MAANA HAIINGII AKILINI KUWA MTU MWENYE AKILI TIMAMU APIGE SIMU MAHALI MUHIMU KAMA FIRE NA KUULIZA UPUUZI. MWINGINE ANAPIGA SIMU KUSEMA ETI ANAMTAFUTA MCHUMBA WAKE WALIYEPOTEANA NA BADO MTU ANAISHIKILIA SIMU KWA MUDA HATAKI KUKATA, JAMANI WATANZANIA WENZANGU HIVI HUU NDO UJANJA WA SIKU HIZI EEEEEE. MNIAMBIE JAMANI MAANA MIMI MNYAMWEZI LABDA SIYAJUI YA MJINI. TUKUMBUKE WAKATI WEWE UMESHIKILIA LINE KWA UPUUZI WAKO KUNA MTANZANIA MWENZAKO SEHEMU NYINGINE ANATEKETEA KWA MOTO, WAKATI WEWE UMESHIKILIA LINE KUNA MTANZANIA MWENZAKO ANAHAHA KUTAFUTA MSAADA POLISI KWA KUWA AMEVAMIWA NA MAJAMBAZI NA NDO YANAKARIBIA CHUMBA CHAKE. HEBU FIKIRIA UTAKAPOKATA SIMU UKAKUTA SMS INAKUAMBIA, "DADA NYUMBA YANGU IMETEKETEA KWA MOTO NA MTOTO WANGU MDOGO AKIWA NDANI, NILIJARIBU KUPIGA SIMU FIRE IKAWA IKO BUSY" UTAJISIKIAJE? WAKATI MWINGINE UNAWEZA UKAWA UNAFANYA HIVYO KUMBE UNAWAHARIBIA MAISHA UNAOWAPENDA WEWE. NIMEANDIKA HAYA KWA HASIRA KIDOGO MAANA NIMESHINDWA KUWATAMBUA WATANZANIA WENZANGU WANA TATIZO GANI. NI UFINYU WA ELIMU AU UGENI NA SIMU ZA BURE? LABDA MAKUSUDI BWANA HAIWEZEKANI IKAWA UFINYU WA ELIMU. YAANI NAJIULIZA MWENYEWE NA KUJIJIBU MWENYEWE. EEEEEH NISIWACHOSHE MWAYA YATOSHA. TUWE WAANGALIFU, WHAT GOES AROUND COMES AROUND. GOOD MORNING.
Aaaaaah mimi huyoo utantaka!!
The one and only Winnie
Ila tuacheni masihara jamani mapozi kazi eeeeeeh.
No comments:
Post a Comment