WAKATI MWINGINE NASHIDWA KUYAELEWA MAISHA YANA MTIRIRIKO GANI, WAKATI KUKU ANAHANGAIKA KULINDA WATOTO WAKE WASIJE WAKANYAKULIWA NA MWEWE AU KUNGURU BINAADAMU MKE ANAHANGAHIKA KUTOA MIMBA NA KUTUPA VICHANGA MTONI. HIVI NI KWELI KWAMBA MWANAMKE WA LEO AMEZIDIWA AKILI NA KUKU TETEA? SITAKI KUKUBALI HILO NA PIA SITAKI KUKUBALI ETI KUWA WANATUPA WATOTO KWA KUWA MAISHA MAGUMU NA BABA WA MTOTO AMEMKATAA. KWANI WEWE MWENYEWE UNAKULA NINI ATAKACHOSHINDWA KULA HUYO MALAIKA WA MUNGU? NAUMIZWA SANA NA HADITHI HIZI. SIMZUNGUMZII MTU KWENYE HILI ILA BAADA YA KUONA PICHA HIYO HAPO JUU NIKAJIKUTA NAKUMBUKIA MATUKIO AMBAYO NILIWAHI KUYASIKIA AU KUYASHUHUDIA YA WADADA KUTUPA VICHANGA MTONI AU CHOONI. KAMA UNAONA HUWEZI KUWA NA MTOTO BASI HAKIKISHA PIA HUWI NA BABA YAKE MTOTO, HILO LITAKUSAIDIA KUKUONDOLEA DHAMBI YA UUAJI. NI MTAZAMO TU MASELA MSIJENGE CHUKI.
No comments:
Post a Comment