MCHANA WA LEO BABA YANGU MZAZI MZEE SYLVESTER ANDREA MALEKELA NGALABA ANATARAJIA KUFANYIWA UPASUAJI WAKE WA PILI WA MACHO. UPASUAJI HUU UNARUDIWA KUTOKANA NA MAKOSA YALIYOFANYWA MWANZO NA MADAKTARI KWA KUZIBA MISHIPA YA MACHOZI. INANIUMA SANA KUMUONA KWENYE ILE BANDEJI NA MAUMIVU ANAYOONYESHA KUWA NAYO USONI INGAWA HATA UKIMUULIZA ANAKWAMBIA "AAAH NIKO VIZURI MAUMIVU NI KIDOGO TU". NAMPENDA SANA BABA YANGU KULIKO NINAVYOWEZA KUELEZEA, HIVYO ANAPOKUWA KWENYE MAUMIVU NA MIMI HUWA NAUMWA ZAIDI, NAOMBA MUNGU AMPUNGUZIE MAUMIVU ILI AENDELEE NA SHUGHULI ZAKE KAMA KAWAIDA KWANI HUWA NAONA ANAVYOKUWA AU KUUMIA SHUGHULI ZAKE ZIKISIMAMA. NAAMINI MUNGU NI MWEMA NA ANAFANYA KILA AOMBALO MJA WAKE. SITARAJII MAKOSA MENGINE TENA KWENYE UPASUJI HUU ILA NATARAJIA UMAKINI WA HALI YA JUU ILI KUREKEBISHA MAKOSA YA AWALI. NATAMANI KAMA HAO MADAKTARI WANGEONA UJUMBE HUU ILI WAWEZE KUJUA KUWA WANAUMIZA WATU WENGI ZAIDI MAKOSA YA AINA HII YANAPOTOKEA. KILA LA KHERI BABA YANGU MPENZI NAJUA MAMA YUPO KWA AJILI YA KUKUSAIDIA.
LOVE YOU ALL.
No comments:
Post a Comment