Tuesday 3 November 2015

SAMAHANI LAKINI, NIMEIPEND HII KITU, MSINICHUKULIE VIBAYA

COPY & PASTE FROM BLOG YA WANANCHI

Kuna jamaa kaja hapa kwangu ananiambia vipi tunaandamana?? 
Eti Kaja kunipitia na mimi alidhani na mimi Nyumbu.


Yeye anashawishi vijana waandamane..
Nikamuuliza wanaandamana kupinga nini? 
anasema matokeo ya urais

Nikamuuliza ya ubunge je?
Akasema hayo hakuna neno wao wanapinga ya urais tu,
Nikamuukiza wana wabunge wangapi na ccm ina wabunge wangapi?
Anajibu kwa ujumla wao wana wabunge kama 72 na majimbo 10 hayajafanya na majimbo 8 wataenda mahakamani na ccm ina zaidi ya wabunge 180.
Nikamwambia ktk wabunge wenu jumlisha 10 na 8 mtakaoenda mahakamani jumla mtakua na wabunge wangapi?
Akaniambia 90.
nikauliza ccm watakua na mangapi? 
Akajibu 174..

Nikamuukiza kwaiyo Lowasa akishinda anaweza kuunda serikali?
Akajibu hapana..
Sasa unaandamana kwa ajili ya selikari ya mseto ama??
Jamaa kimya anasema yeye kaambiwa aandamane tu kupinga matokeo..
Nikamuuliza kwa akili yako umewahi kuona wapi hapa duniani chama kikashinda idadi kubwa kama hiyo ya wabunge wa ccm halafu ikashindwa kwenye urais??
Anaiambia ngoja aingie google atafute..
Nikamuonyesha video kadhaa za Nyumbu
Akaniuliza una maana gani kunionyesha hizi video?
Nikamjibu
‪#‎usiwe‬ kama Nyumbu#..
Akavua gwanda ameenda kulala..

No comments: