Monday, 29 July 2013

REST IN PEACE BROTHER EMIL ISSA KIPANDE, TEACHER

MAREHEMU EMIL ISSA KIPANDE

NI MIEZI SITA TU IMEPITA TOKA ALIPOFARIKI MAMA YETU MPENZI, TUMEPOTEZA TENA MPIGANAJI MWINGINE KATIKA FAMILIA. MWL. ISSA ALIKUWA KAMA MBADALA WA MAMA KWA KILA KITU, YEYE NDIYE KAKA AMBAYE UNAWEZA UKAKAA NAYE AKAKUSIKILIZA NA KUKUSHAURI LINALOWEZEKANA. TUMEPOTEZA KICHWA CHA KUTUSIMAMIA NA KUTUONGOZA KWA MENGI INGAWA KWA UKALI LAKINI ALIKUWA NA MSIMAMO UNAOELEWEKA. EEE MUNGU SIPENDI KUKUFURU LAKINI MBONA UNACHAGUA KWENYE UMUHIMU?? MBONA UNAGUSA SISI TUPOANGALIA ZAIDI?? KWANZA MAMA, SASA KAKA HUONI KWAMBA SISI WENGINE TUTASHINDWA KUENDELEA KUSIMAMA? BAADA YA MAMA YEYE NDIYE ALIKUWA ANGUKIO LANGU LA KWANZA, ALIKUWA MSIKIVU KWA KILA NILICHOKUWA NANUNG'UNIKIA KWAKE NA KUKIFANYIA KAZI. WAKATI MWINGINE NAHISI KAMA NAONEWA JAMANI. JEMBE LETU LIMEONDOKA, BABA MKUBWA MZEE KIPANDE ALIWAHI KUNIAMBIA KWENYE MSIBA AKASEMA "MWANANGU JASIRI AMEONDOKA, MKONGOJO WANGU UMEONDOKA, NITATEMBEAJE MIMI?" HAKUKOSEA KABISA, YEYE ALIKUWA KILA KITU KWETU NA KWA WAZEE WETU PIA. EEEE MWENYEZI MUNGU TUJALIE FARAJA SISI NA MUONGOZO WA UHAKIKA. YULE ULIYETUTAFUTIA KWANZA BAADA YA MAMA NAYE UMEMWITA MBELE ZAKO. TUONGOZE TUJUE WAPI KWA KUSHIKA MUNGU. MTIHANI ULIOTUPA NI MKUBWA SANA NA UPO NJE YA UWEZO WATU. NAKUOMBA SANA MUNGU UMPUNGUZIE ADHABU YA KABURI KAKA YANGU MPENZI EMIL ISSA KIPANDE AKAPATE KUIONJA PEPO YAKO, ILA SI KWA MAPENZI YANGU ILA KAMA UONAVYO WEWE SAWA. PUMZIKA KWA AMANI KAKA YANGU MPENZI.


REST IN PEACE BOTHER, LOVE YOU MUCH

MKE MKUBWA WA MAREHEMU, POLE SANA WIFI YANGU


BINTI MKUBWA WA MAREHEMU, STAMILI EMIL ISSA

BINTI MDOGO WA MAREHEMU, LATIFA EMIL ISSA

SIKUJUA HIZI PICHA NIMEPIGWA SAA NGAPI ILA NIMEKUJA TUMIWA TU,






NYUMBANI KIDODI TULIKOZIKA



REST INI PEACE KAKA YANGU MPENZI

No comments: