Tuesday 2 July 2013

MAPOKEZI YA OBAMA

 Wakina mama wamejitanda na khanga zenye picha ya Barack Obama
 Rais Baraka Obama akicheza ngoma alipokua akipita kwenye moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza kwa ajli ya ujio wake mara tu aliposhuka kutoka kwenye ndege ya Airforce One

 Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete akitabasamu wakati mgeni wake Rais Barack Obama alipokua akitikisa mwili kwa hisia za ngoma za asili zilizokua zikitumbuizwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa ujio wake leo akitokea Afrika ya Kusini.
 Rais Barack Obama akiangalia moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbiza uwanjani hapo.
 Rais Barack Obama akikagua majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais wa Marekani Barack Obama pamoja mkwewe wakilakiwa na mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete mara tu walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere leo Jumatatu July 1, 2013 kwa ziara ya siku 2., kushoto ni mama Salma Kikwete.

Rais Barack Obama wa Marekani (kushoto) akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari wa Tanzania na Kimataifa Ikulu Jijini Dar es Salaam jioni hii ambapo mbali na kuzungumzia mstakabali wa ziara yake nchini Tanzania na Afrika pia amezungumzia masulala mbalimbali ya Kimataifa ukiwepo mgogoro na Vurugu zinazoendelea nchini Misri na Congo DRC.

1 comment:

Anonymous said...

Mh,kweli jasili ahachi asili,amevutiwa na ngoma za kitanzania hadi amecheza,hongera kwa watanzania.