Friday 30 October 2015

MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI RASMI



Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemkabidhi cheti cha ushindi wa kiti cha urais, Dk John Pombe Magufuli na mgombea mwenza wake Samia Suluhu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee asubuhi hii.
Katika tukio hilo, Wagombea urais wa Chadema Edward Lowassa na Hashim Rungwe wa Chauma wamesusia sherehe hizi za kukabidhiwa cheti cha ushindi Dk John Magufuli wa CCM.



 Rais anayeondoka Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria hafla hiyo, sawa na kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan. Bw Jonathan amampongeza rais mteule.

John Pombe Joseph Magufuli akabidhiwa rasmi cheti cha ushindi uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili Oktoba 25.
11:00am: Hafla ya kumkabidhi Magufuli cheti inafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. 

No comments: