Thursday 1 October 2015

USHABIKI RAHA SANA DUH



Njemba huyo akipakwa lipstick.
AHADI ni deni! Njemba mmoja mkazi wa Mbezi Manyema, jijini Dar aliyejulikana kwa jina la Omar Msambaa, hivi karibuni alijikuta akipakwa lipstick, kunyolewa nywele na baadaye kuogeshwa kwa soda aina ya mirinda, ikiwa ni kutimiza ahadi yake ya awali kuwa afanyiwe hivyo endapo timu aliyokuwa akiishabikia itafungwa.Chanzo chetu kililiambia gazeti hili kuwa, awali Msambaa, shabiki mkubwa wa timu ya Simba, alikuwa amejiapiza afanyiwe kitendo hicho mbele ya mjumbe wa mtaa, akitamba kuwa klabu yake haiwezi kufungwa na watoto wadogo kama Yanga.
Baada ya ahadi hiyo, inadaiwa watu walitawanyika kila mmoja akisubiri siku ya mchezo ifike na baada ya ‘mnyama’ kukubali kichapo cha mabao 2-0, Msambaa alitoweka eneo hilo akihofia kufanyiwa kitendo alichoahidi.

…Akinyolewa.
Inadaiwa baada ya siku kama mbili kupita, walitonywa na mtu kuwa Msambaa alikuwa maeneo ya Tatedo, ndipo vijana wakamfuata na kumbeba juujuu hadi kijiweni ambako walianza kutekeleza ahadi zake kwa kumnyoa nywele, kumpaka rangi mdomoni (lipstick) na kana kwamba haitoshi, wakamletea sufuria lililojaa maharage wakampa na mkate na kumlazimisha kula.

No comments: