Tuesday 27 October 2015

MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI




Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Usiku huu imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 27 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo 17 wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo 10Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu tatu, ambapo asubuhi mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.
Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.


Usiku huu majira ya saa mbili , Jaji Lubuva ametangaza majimbo mengine 14 ambapo kati ya hayo majimbo 8 yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo 6 yakionyesha Lowassa anaongoza.
Majimbo hayo ni kama ifuatavyo:
Matokeo ya Urais Singida Mjini
Kura: 56,558
Magufuli (CCM): 36,035
Edward Lowassa (Chadema): 19,007












Matokeo ya Urais Jimbo la Lindi Mjini
Kura: 38,992
Magufuli (CCM): 21,088
Edward Lowassa(Chadema): 17,607


Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini
Kura: 55,772
Magufuli (CCM): 33,626
Edward Lowassa(Chadema):20,368


Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho
Kura:45,374
Magufuli (CCM): 32,505
Edward Lowassa (Chadema): 11,291


Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga
Kura: 39,788
Magufuli (CCM): 23,798
Edward Lowassa (Chadema): 15,142


Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini
Kura:79,814
Magufuli (CCM): 28,909
Edward Lowassa (Chadema): 49,379


Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba
Kura: 44,437
Magufuli (CCM): 24,904
Edward Lowassa (Chadema): 16,992


Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295
Edward Lowassa (Chadema):11,695


Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe
Kura: 38,012
Magufuli (CCM): 24,086
Edward Lowassa (Chadema): 13,093


Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni
Kura: 7,539
Magufuli(CCM):710
Edward Lowassa (Chadema): 6,506


Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe
Kura: 7,620
Magufuli (CCM): 428
Edward Lowassa (Chadema): 6,937




Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho saa tatu asubuhi.


Matokeo Yaliyotangazwa mchana Yako Hapo Chini. Bonyeza Picha Kuyaona Vizuri





























No comments: