Monday 8 October 2012

George Maganga Day

Jana kaka yangu Maganga ilikuwa siku yake kubwa maana ndio ilikuwa siku ya kukubalika au kukataliwa baada ya kupeleka mahari kwa wazazi wa mpenzi wake Gift.


Wapambe nao walikuwepo Joyce,Mesha na Bishagazi

 
Mama mkubwa wa Gift akipokea zawadi waksi doti nne kwa niaba ya mzaa chema

Bibi naye akiwa amejitwisha blanketi lake mgongoni ishara ya kukumbukia alivyombeba Gift

Sehemu ya zawadi zilizokamilisha zoezi letu

Babu naye akipokea chake baada ya kukubali kumuachia mke wake mrembo


Hili ndio lilikuwa zoezi kuu la siku hiyo. Mahari yenyewe, kumtoa mtoto mrembo kama Gift lazima mifuko itoboke

Ma mkubwa akiwa kabeba mahari yetu kuonyesha kuwa tumekubaliwa

Baada ya kukubaliwa mtarajiaa akaitwa kutambulishwa, rahaaajeeee

baada ya utambulisho wakaruhusiwa kupiga picha mbili tatu na kukaa pamoja kubadilishana mawazo

wanapendezeanajeeee

Kaka yangu kajua kuchagua jamani kama hutaki roho yako mbaya tu kwa kuwa wewe malaine



Kama haamini vile hebu muone anavyomuangalia

Mpaka mrembo kagundua ikabidi amwambie dear me wako peke yako pressure ya nini? kuwa na amani sweetie



baada ya zoezi hili tulielekea Chilakale resort kwa ajili ya engagement party. kaa mkao wa picha






2 comments:

Anonymous said...

Kazi nzuri mami.

Anonymous said...

Wale waliodanganywa chalii, maana jamaa huko alikopita alikuwa anaingia kwa gia za kuowa.