Thursday, 1 November 2012

HIZI NDIO PICHA ZA AJALI YA BASI LA ABOOD MBEYA

 Hivi ndivyo basi La Abood lilivyo pata ajali baada ya kugongana na Kenta
 Basi la Abood
 Hivi ndivyo Basi Lilivyo Haribika
 Haya ni mambaki ya Vioo vilivyo vunjika
 
 Baadhi ya vitu vikiwa vimemwagika chini
 
 Hili ni Scania ambalo lilikuwa likitokea Zambia
 Dirisha likiwa lililovunjika
Baadhi ya Abiria wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa polisi
picha zote ni kutoka www.mbeyayetu.blospot.com
BASI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU  KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.
KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA AMBAYE  ANAITWA CHALE KITELEKE AMBAYE PIA ALIKUWA NDIYE KONDA WA BASI HILO AMEFARIKI PAPO HAPO, PAMOJA NA MAJERUHI NANE AMBAO WAMEKIMBIZWA HOSPITALINI .
 

No comments: